Sheikh Mshele alieleza kwa kina tukio la kunyang’anywa Fadak, ardhi ambayo ilikuwa haki na zawadi halali ya Sayyidat Fatima (sa) aliyopewa na Mtume (saww). Alibainisha kuwa tukio hilo limeorodheshwa na wanahistoria wengi na limeacha doa lisilofutika katika historia ya mwanzo wa Uislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlis ya maombolezo ya kumbukumbu ya Kifo cha Sayyidat Fatima Zahra (sa) — Binti kipenzi wa Mtume Muhammad (saww) — imefanyika jijini Arusha, Tanzania, tarehe 25 Novemba 2025. Hafla hiyo imehudhuriwa na waumini wengi waliokusanyika kwa ajili ya kumuenzi Mwanamke bora wa Umma na kutoa heshima kwa nafasi yake tukufu katika Uislamu.
Khatibu wa majlis hiyo, Sheikh Haidary Ally Mshele, alitoa mawaidha yaliyojaa uchungu na mafunzo, akieleza kwa ufafanuzi mkubwa dhulma na mateso aliyoyapata Sayyidat Fatima (sa) muda mfupi baada ya kufariki kwa Baba yake, Mtume Muhammad (saww).

Sheikh Mshele alieleza kwa kina tukio la kunyang’anywa Fadak, ardhi ambayo ilikuwa haki na zawadi halali ya Sayyidat Fatima (sa) aliyopewa na Mtume (saww). Alibainisha kuwa tukio hilo limeorodheshwa na wanahistoria wengi na limeacha doa lisilofutika katika historia ya mwanzo wa Uislamu.
Khatibu huyo alisisitiza kuwa historia kamwe haiwezi kusahau dhulma hiyo, na kwamba Siku ya Kiyama - siku ya kupambanua baina ya haki na batili - madhalimu wote watajua mwelekeo watakaogeuzwa kwa ajili ya matendo yao.
Majlis hiyo, iliyojaa maombi, maombolezo na ibada, ilikumbusha nafasi ya juu, uchamungu, na msimamo madhubuti wa Sayyidat Fatima (sa) katika kutetea haki na kusimama na maadili aliyofundishwa na Mtume (saww).

Your Comment